Saturday, March 11, 2017

Klabu ya soka ya Paris Saint-Germain wameanza mbio za kumuania kumsajili mshambuliaji mahiri Alexis Sanchez wa timu ya taifa ya Chile na klabu ya Arsenal.

Mchezaji huyo ambaye ana umri wa miaka 28, inasemekana hayupo katika mahusiano mazuri kwasasa na kocha wake Arsene Wenger kwaiyo anajiandaa kusepa katika klabu ya Arsenal baada ya kuisha kwa msimu huu kutokana na kutokubaliana na maslahi ya mkataba mpya na klabu hiyo, na Wenger amemuambia kwamba anaweza kuondoka.

0 comments:

Post a Comment