Posted by Williammalecela.com on Wednesday, March 29, 2017
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
hakuhudhuria mazishi ya mwanaharakati wa kuipinga serikali ya ubaguzi wa
rangi Ahmed Kathrada kwa ombi la familia yake. Bwana Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu mwaka uliopita, kufuatia kashfa za ufisadi. Makamu wa rais Cyril Ramaphosa aliiwakilisha serikali kwenye mazishi hayo. Bwana
Kathrada mwenye umri wa miaka 87, aliaga dunia siku ya Jumanne.
Alifungwa pamoja na Mandela kwa kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi. Alitumikia kifungo cha miaka 26 gerezani kabla ya kauchiliwa
mwaka 1989. Baadaye alihudumu kama mshauri ra rais wa zamani Nelson
Mandela, kwenye serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasia. Bwana
Zuma alikuwa ameagiza bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo
chake, na kuhairisha mkutano wa mawaziri ili maafisa wapate kuhudhuria
mazishi yake. Image caption
Bwana Zuma amekataa kujiuzuluHata hivyo Zuma hakudhuria mazishi wala ibada ya maombi kufuatia ombi la familia ya kathrada. Mke wa Kathrada Barbara Hogan anafahamika kuwa mkosoaji mkubwa wa bwana Zuma. Bwana
Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu baada ya mahakama ya juu zaidi nchini
Afrika Kusini, kuamua kuwa alikuwa amekiuka katiba kwa kukataa kulipa
pesa ambazo zilitumiwa kukarabati makao yake ya kibinafsi huko Nkandla.
0 comments:
Post a Comment