Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi kesho amefunga
kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’ kwa makocha 27 waliohitimu kozi hiyo.
Kozi
hiyo iliendeshwa na Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF Wilfred Kidao -), katika uwanja wa Michezo wa Bandari, uliopo
Tandika jijini Dar es Salaam.
Wakufunzi
wengine walikuwa ni Peter Manyika aliyefundisha programu au mtaala kwa makocha wa
makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao kuhusu tiba za
wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.
Wanafunzi
wa kozi hiyo ni Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke pekee kati ya wanafunzi 27
walisoma kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14 cha mwanzo wa mwaka.
Wengine
ni nyota wa zamani wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’
waliopata kuchezea klabu kongwe na kubwa nchini. Wanafunzi hao ni Boniface
Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na
Mussa Hassan Mgosi.
Orodha hiyo
imewajumuisha pia Omar Kapilima, Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho,
George Minja, Haruna Adolf, Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud Selemani, Haji
Mustapha, Mhasham Khatib, Issa Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio
Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.
0 comments:
Post a Comment