Monday, March 13, 2017

Mwendesha mashtaka wa jimbo la Manhattan Preet Bharara amefutwa kazi na Rais Donald Trump.Preet Bharara amesema kuwa hajajiuzulu kama inavyojulikana na wengi bali amefutwa kazi.
Bwana Preet ni kati ya waendesha habari waliochaguliwa na Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions alimshauri Preet pamoja na waendesha mashtaka wengine 45 waliochaguliwa na Barack Obama kujiuzulu.Bwana Bharara alikataa kujiuzulu baada ya Rais Trump kumwambia kuwa anaweza kuendelea kuwa mwendesha mashataka saa chache tu baada ya Rais Trump kuwa Rais mwezi Novemba.

0 comments:

Post a Comment