Wednesday, March 22, 2017


Mshshambuliaji wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy amesema amekuwa akipokea vitisho vya kuuwawa yeye pamoja na familia yake, toka aliekuwa meneja wa klabu hiyo Claudio Ranieri alipofutwa kazi mwezi uliopita.


Vitisho hivyo vimetokana na mashabiki kuhisi kwamba Vardy aliushinikiza uongozi wa Leicester umfute kazi Kocha Claudio Ranieri.

Ranieri alifutwa kazi mwezi Februar, ikiwa ni miezi tisa tu imepita toka alipoipa Leicester taji la ligi ya Premier nchini Uingereza.

Vardy amesema anasikitishwa sana na vitisho ambavyo amekuwa akivipata kwani kila kukicha mambo mapya yamekuwa yakijitokeza na kutolea mfano habari iliyomuhusisha na kukutana na uongozi wa klabu ya Sevilla wakati alipokwenda kufanyiwa vipimo vya kama anatumia dawa zilizokatazwa michezoni.

Nyota huyo ambae aliiwezesha Leicester kutwaa taji msimu uliopita amesema muda mwingine alitaka kukaa kimya na kuamini kuwa haya ni mapito tu lakini alishangazwa na kushtushwa sana wale waliotaka kumfanyia vurugu mke wake wakati akiwa kwenye gari pamoja na watoto wake.

Shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC limeeleza kwamba baadhi ya nyota wa klabu hiyo walijaribu kuzungumza na uongozi mara baada ya kukamilika kwa mchezo dhidi ya Sevilla katika ligi ya mabingwa na kupoteza kwa mabao 2-1 ili kimtetea kocha Claudio Ranieri lakini uongozi wa klabu hiyo haukukubaliana na mtazamo wa wachezaji hao.

Mara baada ya ranieri kuondoka, mikoba yake ilichukuliwa na aliekuwa msaidizi wake Craig Shakespeare ambae sasa ataiongoza Leicester hadi mwishoni mwa msimu.


Katika michezo mine ambayo Shakespeare ameiongoza Leicester hadi sasa imefanikiwa kupata matokeo katika michezo mine mfululizo na hivyo kusogea hadi katika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi kuu soka nchini Uingereza pamoja na ushindi katika ligi ya mabingwa ulioiwezesha kutinga katika hatua ya robo fainali.

0 comments:

Post a Comment