Saturday, March 4, 2017

Kama umefollow page ya @perfectotv  kwenye instagram naamini jana ulikutana na post iliyoonyesha comment ya Youg Killer kwenye post ya Dogo Janja.

Post ambayo Janja alitupia picha akionyesha Ndinga yake mpya ambayo kanunuliwa na management yake baada ya kupata majanga ya kuibiwa kila kitu kwenye gari yake ya awali.
Kama ulipitwa na kisanga hicho embu pitisha macho hapa chini.

Baada ya watu kufuata mkumbo wa Young Killer na kumzonga sana Dogo JanjaJanja akaona sio kesi na kuamua kuitupia kadi ya gari yake hiyo kwenye mtandao.

Sasa baada ya sakata lote hilo, Perfect255 ikaona sio kesi, tumemtafuta Janja na kumuweka kwenye exclusive interview na amefunguka mengi kuhusiana na Young Killer.
“Unajua hawa watoto wanajuaga kama mimi ni kama mwanamke, yaani wale wanawake wanaopewa magari halafu kadi hawapewi. Yule mtoto ni mshamba mshamba halafu ni mtoto mdogo. Ni mtu ambaye ukibishana naye utapigizana naye kelele.”
Hicho ni kionjo cha POVU ambalo Dogo Janja amemtoleaYoung Killer, sasa kulisikiliza POVU kamili bonyeza play kwenye video hii hapa chini.

0 comments:

Post a Comment