Wednesday, March 1, 2017

kuna wakati hivi unamkosea mtu then unajiuliza kwa mtakutana kwenye lipi? Kama vipi unaona binadamu ni milima na haisogei! Kaa hivyo hivyo baada ya Rais wa Manzese aliyehamia Kimara  Ney Trueboy kumchana sana katika baadhi ya ngoma zake aliyekuwa Shemela  wake wa zamani kwa mshikaji wake Chibu katika baadhi ya ngoma zake kadhaa mrembo Wema Sepetu.

Unaambiwa wawili hao kwasasa ni damdam wamekuwa washikaji baada ya kukutana katika chimbo jipya ambalo Wema amejimuvuzish ndani ya CHADEMA kule amekwenda kukutana na Ney Wa Mitego ambaye amemkaribisha kwa mikono miwili kiroho safi washirikiane kujenga  Chama chao.
Mapema leo Ney alitupia picha kwenye Ukurasa wake wa Instagram na Twitter aimkaribisha rasmi Sepenga chamani.
Na Bonge la Caption ilikuwa inasomeka hivi “Wana maneno mengi Tatizo hawana action, usimuamini ndugu hata rafiki ishi utakavyo binadamu hawaaminiki” then akamalizia na Bonge la hashtag #MudaWetu

0 comments:

Post a Comment