Tuesday, March 7, 2017

Kitaani kuna tetesi ambazo zilienea kuwahusu wakali wawili wa filamu nchini Vicent Kigosi (Ray) pamoja na mwanadada Johari kuhusu kuvunjika kwa kampuni yao ya RJ COmpany.

Mengi yaliongelewa kuwahusu wawili hao na wengine kwenda mbali zaidi na kudai kuwa wawili hao hawana maelewano tena kama zamani kutokana na uhaba wa movies ambazo zinawakutanisha wawili hao kama zamani.
Ijumaa iliyopita Vicent Kigosi alikuwa anaizindua rasmi movie yake mpya ambayo kaipachika jina la Gate Keeper, movie ambayo imeanza kuingia sokoni rasmi leo jumatatu ya March 6.
Ndipo ambapo kipaza cha Perfect255 kilisogezwa karibu na Ray Kigosi na kumtaka aweze kulizungumzia suala hilo la ugomvi wa yeye na Johari.
“Unajua siku zote Watanzania huwezi kuwazuia kuzungumza, RJ ni brand ya watu wawili yaani Ray na Johari, labda wanasema hivyo kwasababu hawajamuona Johari akiigiza kwa muda mrefu. Unajua sisi Watanzania tatizo ni moja, nikicheza na Johari kila siku watasema ah, Ray bhana kila siku anacheza na Johari, ukisema umpumzishe Johari watasema kwanini Ray hachezi na Johari, basi kampuni inaelekea kufa. Kwahiyo watanzania huwezi kuwaridhisha, fanya kitu ambacho unaona kiko sahihi. Kampuni haijafa kampuni ipo.” Alisema Ray Kigosi.

0 comments:

Post a Comment