Roger Federer atakutana na Rafael Nadal katika
michuano ya wazi ya BNP hatua ya nne, hii ikiwa ni mara ya pili kwa nyota hao
kukutana kwa mwaka huu mara baada ya kukutana katika fainali ya michuano ya
wazi ya Australia.
Federer
amesema amekwenda katika michuano hiyo ili akutane na Rafael Nadal kwani
upinzani ambao amekuwa akiupata unamjenga sana na kumfanya awe fiti zaidi.
Katika michuano
ya wazi ya BNP Nadal ambae anashikilia nafasi ya tano kwa ubora duniani
amefanikiwa kufika katika hatua ya nne mara baada ya kumshinda Mhispania
mwenzake Fernando Verdasco kwa seti 6-3 7-5.
Kwa upande
wa Mswis Roger Federer, ambae hadi sasa ameshatwaa mataji 18 ya Grand Slam amefanikiwa
kufika katika hatua ya nne mara baada ya kumshinda Steve Johnson wa Marekani
kwa seti 7-6 7-6.
Nyota mwingine
katika mchezo wa tennis Novak Djokovic amefanikiwa kumshinda Juan Martin del
Potro.
Mara baada
ya Djokovic 6-kupita katika hatua hiyo, sasa atakutana na Nick Kyrgios, toka Australia ambe
kwa viwango vya ubora anashika nafasi ya 18.
0 comments:
Post a Comment