Timu ya Taifa ya Tanzania kwa wanandinga wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys leo tarehe 30 March imefanikiwa kuilaza Burundi kwa mabao 3-0 katika mchezo wa maandalizi ya kwenda Gabon kwenye AFCON uliopigwa Kaitaba -Bukoba.
Katika mchezo huo uliokuwa wenye kasi na wa kuvutia, mabao ya Serengeti Boys yaliwekwa kambani na Muhsin Malima Makame 20', Nickson Kibange 38', pamoja na Yohana Mkomola katika dakika ya 72 kupitia changamoto ya mkwaju wa penat.
Serengeti Boys itakuwa kambini huko Bukoba hadi Aprili 2, chini ya Kocha Bakari Shime ikiwa imeweka kambi ya juma moja na sasa itarudiana tena na Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, Aprili mosi, mwaka huu.
Timu hiyo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon na itarejea jijini Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezoambao utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Timu itaelekea Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye itapita Cameroon kwenye kambi ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon katika michuano itakayoanza Mei 14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.
0 comments:
Post a Comment