Kikosi
cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys
kimeendelea na mazoezi huko Bukoba mkoani Kagera kikijiandaa kwaajili ya
michezo miwili ya kujipima nguvu kalba ya kuelekea katika kambi ya nje ya nchi
na baadae kuelekea Gabon katika fainali za Afcon kwa vijana wenye chini ya
miaka 17.
Katika mahojiano maalum na Blogu ya Jamii, kocha mkuu wa Serengeti
Boys Bakari Shime amesema mazoezi yameendelea vema na anategemea kupata matokeo mazuri katika michezo ya kirafiki.
Mara baada
ya kukipiga katika michezo hiyo miwili Serengeti Boys itarejea jijini Dar es
Salaam Aprili 2, na kukipiga dhidi ya Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo ambao utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa
kukabidhiwa bendera.
Kabla ya kwenda Morocco Serengeti boys itaweka kambi
ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye nchini Cameroon na baadae itakwenda Gabon
katika michuano itakayoanza Mei 14, 2017.
Ikiwa
Cameroon itacheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya wenyejiCameroon kabla ya
kwenda kwenye fainali.
Serengeti Boys imepangwa katika Kundi ‘B’ pamoja na
mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola na endapo itafanikiwa kumaliza katika
nafasi mbili za juu katika Kundi hilo itkuwa imekata tiketi ya kushiriki katika
fainali za Kombe dunia kwa vijana huko India, Novemba, mwaka huu.
Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na
Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin Kayego.
Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson
Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick
Vitalis Nkosi.
Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi,
Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman,
Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.
Washambuliaji: Muhsin Malima Makame, Yohana
Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
0 comments:
Post a Comment