Jana mahakama jijini Dar es Salaam ilimhukumu Jangili nguli kutokea nchini Tanzania kifungo cha miaka 12 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuunda mtandao wa biashara haramu ya pembe za ndovu barani Afrika.Kwa mijibu wa PAMS Foundation – Conservation ya nchini Tanzania ambayo hufadhili serikali kuweza kupambana na ujangili, Boniface Mathew Maliango maarufu kwa jina la Shetani ni jangili nguli aliyehusika na mauaji ya tembo zaidi ya 1,000 huku akiwa amefanikiwa kuepuka kifungo mara kwa mara.Jangili huyo anayeaminika kuwa ni mkubwa zaidi Afrika Mashariki, alikamatwa Oktoba mwaka jana baada ya kuwa amewindwa kwa muda mrefu bila mafanikio.Inaaminiwa kuwa amehusika kwenye mauji ya maelfu ya tembo akiwa na vikundi vya ujangili katika nchi zote za Afrika Mashariki pamoja na Zambia, na Msumbiji.
Pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyekuwa akihusika na biashara ya pembe za ndovu na raia wa China, Yang Fenlan maarufu Malkia wa Pembe za Ndovu anayeshikiliwa nchini kwa tuhuma za kuuza pembe 706 kati ya mwaka 200o na 2014.Wakati Maliango anakamatwa, alikuwa na pembe za ndovu 118 zenye thamani ya TZS 1,923,390,000.Hukumu hiyo iliyotolewa jana ni kesi moja kati ya nne zinazomkabili. Magari yake matatu yaliyokamatwa bado yanaendelea kushikiliwa kwa kuhusika kwenye shughuli za ujangili.Tanzania ambayo ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya tembo barani Afrika imekuwa ndiyo nchi iliyoathirika zaidi na ujangili. Kati ya mwaka 2009 hadi 2014, tembo nchini Tanzania walipungua kwa asilimia 60.
0 comments:
Post a Comment