Muigizaji
wa filamu nchini, Jacqueline Wolper amemkingia kifua mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwataka watu kuacha kumwandama kwa kashfa
yake ya kufoji vyeti pamoja na kumtukana mtandaoni.Kwa wiki kadhaa
sasa, Makonda amekuwa akiandamwa mtandaoni kutokana na tuhuma kuwa jina
analotumia si lake, na kwamba lake ni Daudi Bashite. Jumapili hii
kumesambaa video mtandaoni ikimuonesha mkuu huyo wa mkoa akilia kwa
uchungu kanisani baada ya kuzungumza na mchungaji akimbembeleza.“Nimevaa
kiatu chake kimenibana mpaka kinataka kunipasua kisigino,” ameandika
Wolper kwenye Instagram.“Jamani wa Tanzania tuwe na utu, acheni
kumtukana huyu kaka daaaah hivi ni nani ambae yupo perfect mpk aanze
kumtukana kaka wa watu jmn. Nimepost nikiwa km binadam wa kawaida ambae
nina moyo!muhurumieni kaka watu acheni Mungu awe muhukumu basi,”
ameongeza.Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote,
Basi hiiKampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...
Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

0 comments:
Post a Comment