Timu
ya taifa ya Tanzania katika mchezo wa Kriket imeendelea na mazoezi ili kujiweka
fiti kuelekea katika mashindano ya mabingwa wa Afrika ICC Afrika Championship ytakayofanyika
Afrika kusini.
Kamera
ya Mbungi ya Afrika Swahili Tv imewashuhudia baadhi ya wachezaji walioitwa
katika timu hiyo wakiendelea na mazoezi ambayo hufanyika asubuhi na jioni.
Timu
hiyo inanolewa na Juan Maitre ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo na sasa ina
kibarua cha kuhakikisha inatetea taji hilo.
Kabla
ya kuanza kwa michuano hiyo Tanzania itacheza kwanza michezo kadhaa ya
kirafiki.
Mataifa
yatakayoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Nigeria, Botswana, Zambia,
Sieara Leone, Ghana na Tanzania.


0 comments:
Post a Comment