Sunday, March 26, 2017

Leo march 26 wapenzi wa burudani nchini Tanzania wameamka na habari ambayo siyo nzuri ikihusu kukamatwa kwa msanii wa kizazi kipya Nay wa Mitego.

Huku tetesi zikidai kuwa kukamatwa kwa msanii huyo huenda inatokana na wimbo ambao ulivuja siku chache zilizopita uliofahamika kwa jina la Wapo. Wimbo ambao alisikika rapper huyo Nay wa Mitego na kusemekana kuwa ndani ya wimbo huo amewachana viongozi wa serikali.
Jambo hilo la kukamatwa kwa Nay wa Mitego limewagusa wengi hususan wasanii wenzake wa muziki.
Nimekusogezea posts za wasanii 5 ambao wameguswa na tukio hilo na kuamua kuandika katika kurasa zao za mitandao ya kijamii kuhusiana na issue hiyo.

Nakupa nafasi na wewe kuniandikia yakwako ya moyoni kupitia uwanja wa comments hapa chini kuhusu kukamatwa kwa Nay wa Mitego.

0 comments:

Post a Comment