Akizungumza na Mbungi ya Afrika Swahili Tv Afisa Habari wa Shirikisho la mchezo wa sooka nchini TFF Alfred Lucas amesema tayari TFF imeshapokea barua kutoka katika Shirikisho la mchezo wa Soka barani Afrika CAF likithibitisha kwamba wanandinga wa Serengeti Boys wana umri sahihi.
Wanandinga hao walifanyiwa vipimo hivyo jijini dar es Salaam na Daktari Pedro toka CAF ili kuepuka gharama za kufanyia vipimo hivyo nchini Gabon.

Katika hatua nyingine Alfred amesema kikosi cha Serengeti Boys kimeendelea na mazoezi kikijiandaa kwa michezo miwili ya kirafiki itakayofanyika katika kanda ya ziwa na baadae kwenda katika kambi ya nje ya nchi kabla ya kuelekea Gabon.
0 comments:
Post a Comment