Thursday, March 9, 2017


WANAWAKE nchini wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo.


Wito huo ulitolewa na Janet Ezekiel Afisa Uhusiano Mwandamizi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia, ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam, yalifanyika katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke.



Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake kitaifa ni "Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi". 

Alisema kauli mbiu hiyo inaenda sambamba na PPF inavyowajali wanawake kwa kutoa mafao mbali mbali yakiwemo ya uzazi pindi anapojifungua mwanachama wa kike anapata kiasi cha shilingi 1,000,000, vilevile alisema PPF inaunga mkono juhudi za Serikali za kuwakomboa wanawake katika kuwawezesha kupata mikopo ya kuendesha biashara zao.

Alisema PPF kupitia mfumo wa Wote Scheme unatoa fursa ya mikopo kupitia benki ya Posta kwa riba nafuu, ambapo wanachama wao hukopa na kuendeleza shughuli zao mbalimbali.

Janet alisema mwanachama mwanamke anaweza kukopa fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara yake na kutoa ajira kwa wengine.

"Kupitia mikopo hiyo, wanachama wanawake wa  Mfuko wa PPF, wanaweza kukopa na kufanyabiashara ziatakazowakwamua kiuchumi na kujitengenezea ajira," alisema.

Aliwataka wanawake kuendelea kujiunga na Mfuko huo ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali zinazopatikana ambazo zitawakwamua kiuchumi na kujitengenezea ajira.

0 comments:

Post a Comment