Waziri Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameunda kamati Maalum ya kuchunguza kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuvamia Ofisi za Clouds Media Group, kwa lengo la kushinikiza habari yake irushwe katika kipindi cha De’ Weekend Chat Show (Shilawadu).
Waziri Nape (kulia) akizungumza na wanahabari mapema leo alipotembelea ofisi za Clouds Media, pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga. Aliyeketi kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Mzee Reginald Mengi.
Waziri Nape amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa saa 24 na baada ya hapo, itatoa ripoti kwa waandishi wa habari na kila kitu kitaanikwa hadharani.
Huu ni mwendelezo wa sakata la mkuu wa mkoa, kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds FM.
TAZAMA VIDEO HAPA



0 comments:
Post a Comment