Licha ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, nahodha wa Leicester City, Wes Morgan ameweka historia mpya katika ligi hiyo kubwa Ulaya inayoshirikisha vilabu.Morgan ameweka historia hiyo wakati timu yake ilipokutana na Sevilla katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Leicester iliibuka na ushindi wa goli 2-0.
Katika mchezo huo, Morgan alifuna goli la kwanza katika dakika ya 27 akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na Riyad Mahrez na goli la pili likifungwa na Marc Albrighton katika dakika ya 54.Goli ya Morgan limemfanya beki huyo wa kati kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Jamaica kufunga goli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League)
0 comments:
Post a Comment