Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo ambavyo hofu inazidi kutanda kwenye nyoyo za Watanzania wote kutokana na ambacho kimewatokea wasanii wa kizazi kipya Roma Mkatoliki na Moni Centrozone.Kila mtu anajitahidi kupaza sauti kadri awezavyo kuhakikisha suala hili linapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo, sababu hakuna anayefahamu kinachowakuta wasanii hao kwasasa.
imepiga story na Nancy ambaye ni Mke halali wa msanii Roma Mkatoliki na amefunguka mengi kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuhadithia jinsi alivyopokea yaarifa hizo za kutekwa kwa Mume wake.“Mara ya mwisho kuwasiliana na mume wangu ilikuwa jana jioni na aliniaga kuwa anaelekea Tongwe Records kwaajili ya kazi zake za kila siku, baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu na me nikachukulia kama ni kawaida tu labda simu imezima nikalala zangu.”
Kuendeleza alichokiongea Nancy bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kumsikia akifunguka mwanzo mpaka mwisho.
0 comments:
Post a Comment