Aliyekuwa
Mke wa Muimbaji wa Muziki wa Injili Emmanuel Mbasha, Flora Mbasha aka
Madame Flora, anatarajia kufunga ndoa na mume wake mtarajiwa Daudi
Kusekwa katika bustani za hoteli ya Rock Beach jijini Mwanza.
Madame
Flora alisema kuwa ndoa hiyo itaambatana na uzinduzi wa albamu yake
mpya inayoitwa ‘Wakati Wake’ pamoja na kitabu alichokipachika jina la
‘Siri za Flora Mbasha.’“Ndoa itafungwa asubuhi na jioni kutakuwa na
sherehe ya harusi, utambulisho wa albamu yangu mpya pamoja na kitabu
kipya. Watu wote wanakaribishwa, ingawa kadi zimebaki chache tu kutokana
na idadi ambayo imepangwa na kamati,” alisema Flora.
Chanzo Mtanzania.
Chanzo Mtanzania.
0 comments:
Post a Comment