Tuesday, April 18, 2017

Mtayarishaji wa video za muziki nchini ambaye kwa sasa anafanya kazi pamoja na rapa Darassa, Hanscana amefunguka kuzungumzia ujio mpya wa rapa huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Muziki’.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Hanscana amedai Darassa alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini ameshindwa kutokana ratiba za show za kimtaifa kumbana.
“Kusema kweli alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini show za Rwanda na Burundi zimembana sana, amekuwa na tour ndefu sana katika nchi hizo na pia baadae ataenda Kenya,” alisema Hanscana. “Tour zikiisha tu ataachia kazi mpya kwa sababu ndani tuna kazi nyingi kali, nikitendo cha kuzitoa tu,”
Hanscana amedai rapa huyo tayari ameshashoot video kadhaa za nyimbo zake ambazo hajazitoa.
Rapa huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya kitendo ambacho kimewafanya mashabiki wa muziki kumsubiria kwa hamu.

0 comments:

Post a Comment