Akiongea na Bongo5 wiki hii, Harmorapa amedai vitu vingi anavifanya katika hali ya kawaida lakini vinakuzwa na media hali ambayo amedai kwake haoni kama ni tatizo.
“Nawaona sana watu wanavyosema mimi ni mtu wa kiki, lakini mimi siyo mtu wa kiki, kiki zinanifuata zenyewe,” alisema Harmorapa.“Mimi naweza kufanya kitu cha kawaida ambacho hata msanii mwingine anaweza kufanya lakini cha kushangaza, kwangu kitaonekana ni kitu kikubwa sana. Kwa hiyo mimi naona ni kutokana na jinsi watu wanavyonichukulia lakini siyo kwamba natengeneza kiki,”Rapa huyo amedai tayari ameshaanza kuona mwanga katika maisha yake ndani ya kipindi kifupi toka aanze muziki
0 comments:
Post a Comment