1: Marekani na Mexico
Hizi ni miongoni mwa nchi zenye migogoro ya kisiasa duniani, lakini migogo hiy haijawazuia wananchi wa nchi hizo kufurahi pamoja. Picha ikionesha wananchi wa Marekani na Mexico wakicheza mchezo wa Volleyball kupitia uzio unaotenganisha nchi hizo mbili.

2: Slovakia, Austria na Hungary
Miongoni mwa mipaka inayovutia duniani ni kati ya nchi hizi tatu ambapo imewekwa meza na viti kwenye mpaka huo kama ishara ya umoja na mshikamano wa nchi hizo.

3: Uholanzi na Ubelgiji
Mpaka unaotenganisha nchi hizi ni miongoni mwa mipaka inayovutia watu wengi ambapo kwa kukadiria kuna umbali wa mita moja kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

4: Sweden na Norway
Ni nchi ambazo hazina migogoro ya kivita, hivyo zinatenganishwa na barabara tu.

5: Ujerumani, Poland na Jamhuri ya Czech
Kiwanja hiki cha kucheza mchezo wa golf ndio miongoni mwa mipaka inayotenganisha nchi nyingi zaidi duniani ambapo Ujerumani, Poland na Jamhuri ya Czech zinapakana na uwanja huu unaonesha kila nchi inapoishia.

6: Uhispania na Ureno
Hii inaweza kukushangaza zaidi, lakini mpaka unaotenganisha kati ya nchi hizi mbili ni waya.

7: Marekani na Canada
Marekani na Canada ni nchi zenye ushindani mkubwa sana hasa kiuchumi, lakini kuna baadhi ya nyumba ambazo zipo katikati ya nchi hizo mbili, hivyo kuzifanya nyumba hizo kujigawa.

0 comments:
Post a Comment