Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
Mwandani
wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari
The Boss Lady’ ameorodheshwa kwenye listi ya watu maarufu nchini Uganda
ambao ni wanachama wa jamii ya siri ya Freemason kisa kikielezwa kuwa ni
utajiri alionao wenye maswali mengi.
Habari
kutoka Kampala, Uganda zilizoripotiwa hivi karibuni zilieleza kwamba,
mwanamama huyo ana ukaribu mkubwa na matajiri wa Nigeria ambao
wanaaminika kuwa utajiri wao ulitokana na kuwa ‘memba’ wa mtandao huo
mkubwa duniani.
Gari la Zari.
Ilidaiwa
kwamba, Zari amekuwa akifanya kufuru ya fedha zinazowashangaza wengi,
kuwa kwa muziki au biashara gani anazofanya zinazomuingizia mkwanja
mrefu kiasi cha kumiliki magari ya kifahari kama Lamborghini na Hummer
ambayo yote ameyaandika majina yake badala ya namba za usajili.
Katika
habari hiyo, wengine waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa mumewe aliyezaa
naye watoto watatu, Ivan Semwanga, wachungaji maarufu nchini humo na
wanamuziki kama Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’ na Bebe Cool.
Zari
anayemiliki hoteli ya kifahari iliyopo kwenye Mtaa wa Kagwa, Kampala
nchini Uganda, anasemekana kumiliki vyuo vya urembo na maduka ya
vipodozi nchini Afrika Kusini huku akijiingizia mkwanja kupitia shoo
zake za Zari All White Party anazozifanya kwenye nchi za Afrika
Mashariki za Uganda, Tanzania na Kenya.
Ijumaa
Wikienda lilipomtafuta Zari hakupatikana badala yake aliyezungumzia
ishu hiyo ni mpenzi wake, Diamond ambaye alisema kuwa mama mtoto wake
ana miradi mingi na siyo kama wanawake wa mjini ambao wanabweteka badala
ya kutafuta mkwanja.
0 comments:
Post a Comment