Saturday, April 15, 2017


Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Bw. Tito Haule ameivunja bodi ya shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) na kuisimamisha kazi menejimenti ya shirikisho hilo, baada ya kubainika kuwepo kwa ubadhirifu.

Uamuzi huo ameutoa mjini Dodoma, kwenye mkutano mkuu wa (TFC), ambapo waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba alishuhudia, ambapo awali wajumbe wa mkutano huo walitaka bodi iendelee na kazi, pamoja na dosari zilizobainika.

Kwa upande wake, Waziri Tizeba alichukua wasaa huo kuwaambia wajumbe wa mkutano mkuu huo kuwa, umefika wakati sasa vigezo vya kuongoza ushirika vikabadilishwa, ili viendane na wakati.

Akiwasilisha taarifa ya uchunguzi, kaimu mrajisi msaidizi, Bw. Revocatus Nyagilo amesema kuptia uchunguzi huo walibaini kasoro nyingi za kiutendaji, na upotevu wa mali za shirikisho.

0 comments:

Post a Comment