Saturday, April 22, 2017

Msanii Diamond Platnumz na team yake wanaizindua rasmi bidhaa yao ya perfume (Chibu Perfume) tayari kabisa kwa kuiingiza sokoni.

Ikiwa hatua hiyo inatazamwa kwa jicho lingine kabisa kufanywa na Mtanzania huyo, ikiwa ni katika kutazama na kuzitumia fursa.
Wengi wamempongeza Diamond kwa hatua hiyo, akiwemo mchekeshaji na mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan baada ya kuandika ujumbe mrefu katika ukurasa wake wa instagram akimsifia Diamond juu ya jambo hilo.
Kupitia instagram, Idris ameandika “Congratulations kwako mshkaji wangu kwa this new brand. Binafsi nipo tayari kununua your brand kwasababu I believe in you and your hustle 
.. Kuna mastaa wengi lakini wengi hujui hata wanafanya nini na umaarufu wao there’s just no content kabisa 
.. God bless your hustle & your beautiful family. Cc: @diamondplatnumz … Kumbuka Vita sio ya sisi wenyewe kwa wenyewe maana mshindi atakua anaongoza kwenye kundi la wazembe. Vita ni sisi na nchi nyingine kuonyesha the real Tanzania .. Nudia “Content muhimu” .. Umetatua tatizo la harufu braza 

0 comments:

Post a Comment