Ikiwa imepita mieizi mitatu tangu Jeniffer Lopez (47) kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi na Alex Rodriguez (41) inaripotiwa kuwa sasa anataka kufunga ndoa na mwanaume huyo.
Mtu mmoja ambaye anaripotiwa kuwa karibu na wapendanao hao aliuambia mtandao wa US Weekly kuwa Jennifer Lopez amewambia kwa sasa yupo tayari kuingia katika maisha mapya ya ndoa.
“Wanazungumza kuhusu maisha ya baade, ni ndoa na mengine yatakuja baadae,” alisema na kuongeza “Hawazungumzi kuhusu harusi ila maisha ya baadae zaidi.”
Aidha inaripotiwa kuwa Jennifer na Alex wameshatambulishana kwa familia zao na kwa upande wa Jennifer, mama yake na dada yake wamesharidhia wawili hao kufunga ndoa.
0 comments:
Post a Comment