Mwanamume
mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao
mjini LondonNaveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake
ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.
Mwili
wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani
kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.Uchunguzi wa kifo chja
mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa
kisu na kisha kukatwakatwa.
Tahira
Ahmed alipatikana akiwa amechinjwa nyumbani kwao mjini LondonBwana
Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old
Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.


0 comments:
Post a Comment