Mbunge
wa Kigoma mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe
amefunguka na kusema atapeleka hoja binafsi bungeni kulitaka Bunge
kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vya utekaji, uteswaji na hata mauaji ya
raia
Zitto
amesema vitendo hivyo vinahusisha pia suala la kijana Ben Saanane
ambaye mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita amepotea na haijaulikana wapi
alipo.
Amesema
hayo leo bungeni wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
mwaka 2017/18 ambapoi amesema kutoweka kwa Ben Saanane kunahusishwa na
watu wa usalama wa Taifa.
"Kuna
kijana wa kitanzania, ndugu Ben Saanane amepotea kwa zaidi ya miezi
mitano sasa. Hajulikani alipo. Wazazi wake na rafiki zake wamemtafuta na
kutoa malalamiko bila mafanikio. Wamefikisha taarifa kwa jeshi la
polisi na wamepaza sauti bila kuchoka. Kuna nyakati suala hili
lilionekana la siasa na ndiyo maana wengine tulikaa pembeni. Lakini sasa
ni miezi 6, hakuna taarifa juu ya suala hili, nimeona nisikae kimya juu
ya hili. Taarifa zinatoka chini chini, siyo rasmi, kwamba huyu kijana
'ametoweshwa'. Kwamba alishikiliwa na watu wa Idara ya Usalama na
amepotezwa. Jeshi la Polisi wana taarifa za mawasiliano ya mwisho ya Ben
Saanane kwa kutumia simu yake ya mkononi, ambayo inaonekana simu
ilipoteza mawasiliano akiwa maeneo ya Buguruni siku aliyotekwa tarehe
15/16 Novemba 2016 na tangu siku hiyo hapakuwa na mawasiliano tena." alisema Ziito Kabwe
Ben Sanane
Mbunge
Zitto Kabwe anasema kuwa matukio ya utekwaji, uteswaji yamekuwa
yakitokea tangu huko nyuma lakini polisi wamekuwa wakikaa kimya na mpaka
leo hakuna hata mmoja ambaye alikamatwa kuhusiana na mambo hayo.
"Kumekuwa
na matukio ya namna hii mabaya kabisa huko nyuma; ndugu Absalom
Kibanda, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri alivamiwa na
kuumizwa vibaya sana na leo jicho lake moja halioni mwaka 2013. Pia
ndugu Yona wa Temeke alitekwa na kuumizwa na kutupwa huko Mbweni jijini
Dar es salaam na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa juu ya matukio yote
hayo. Orodha ya matukio ya namna hii ni ndefu. Watanzania
wamesahaulishwa yote haya, Polisi mpaka leo hawajamkata hata mtu mmoja
juu ya yote hayo". Alisema Zitto
Kutokana
na mambo haya Zitto Kabwe amekusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili
bunge liweze kuunda kamati na kuchunguza mambo hayo ambayo anasema
yanaleta chuki dhidi ya wananchi na taasisi ya TISS.
"Mambo
haya maovu yanayohusishwa na Idara hii yanaondoa uhalali wa Taasisi hii
kwa wananchi, yanaondoa heshima, hadhi na uaminifu juu ya idara hii,
yanajenga chuki na taswira hasi ya Wananchi kwa idara hii, hili si jambo
jema kwa taifa. Ni wakati sasa wa kuchukua hatua. Ni lazima Bunge
liamke na kukomesha hali hii. Kwa mujibu wa Kanuni ya 120(2) ya Kanuni
za Bunge natoa taarifa kwamba nitatoa hoja binafsi kutaka Bunge lako
Tukufu kuunda Kamati Teule kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vya utekaji,
uteswaji na hata mauaji dhidi ya raia (suala la Ben Saanane likiwemo)" alisema Zitto Kabwe
0 comments:
Post a Comment