
Tembo wa bara la Afrika
Tembo ni mnyama kubwa kuliko wote lakini sio mrefu kama twiga, kuna aina mbili ya tembo. tembo wa bara la Afrika na bara la Asia
Ukitaka
kujua tofauti zao wa bara la Afrika ni wakubwa ,na maskio yao
yanamuonekano wa ramani ya bara la afrika lakini tembo bara la Asia
wanamasikio madogo na pia wanaweza kufundishwa kulima na michezo
mbalimbali

Tembo wa Asia.
Akizungumza
na waandishi wa habri kuhusu mnyama huyo (Tembo)Afisa wa shirika la
Tanapa katika hifadhi ya Mikumi Abdalla Choma alisema kuwa Tembo hao wa
wa bara la Afrika wapo katika makundi mawili,
1. Tembo wa msituni wanameno ambayo yamenyooka kwaajili ya kuwawezesha kupita katika msitu
2.
Tembo wa Savana, meno yao yamepindapinda wanapenda kuishi katika
familia moja wanaweza kuishi kwanzia wawili hadi 45 kwa familia
Alisema Tembo wauwezo mkubwa wa kusikia na wanakumbukumbu ya kutosha.
Akizungumzia
kuhusu uzazi wa tembo mzee Chuma alisema kuwa tembo wanauwezo wa kubeba
mimba na kuzaa kwa miezi 18-20Tembo huyo hunyonyesha motto wake kwa
takribani miaka miwili hadi mitatu na motto wa tembo huyo akishafikisha
miaka 15 huesabika ameshakuwa na kutakiwa kuondoka katika familia hiyo
na kwenda kujitegemeaTembo huishi kwa miaka 60-75 kwa sasa lakini miaka
ya nyumba walikuwa na uwezo wa kuishi miaka 80-120 .
“Sababu za kuishi miaka michache kwa miaka hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi “alisema mzee Mchoma
CHAKULA CHA TEMBO
Anapenda kula matawi ya miti na nyasi za chini alafu anakula kwa maasaa 16 kati ya masaa 24
Kiasi cha chakula anachokula ni kati ya 150-300 kg kwa tembo mkubwa na hunywa maji kati ya lita 200 hadi 250
0 comments:
Post a Comment