Saturday, April 22, 2017

Watu wasiojulikana wakiwa na bastola wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao unamuunga mkono, Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na kushusha kipigo kwa baadhi ya wananchama wa CUF na waandishi wa habari.

Mkutano huo wa Profesa Ibrahim Lipumba ulipangwa kufanyika katika hoteli ya Vina, Mabibo majira ya saa tano za asubuhi leo lakini kabla ya kuanza kwa mkutano huo waliibuka watu wasiojulikana wakiwa wamevalia soksi nyeusi usoni kuficha sura zao na kususha kipigo kwa baadhi ya wanachama wa CUF waliokuwepo katika eneo hilo na waandishi wa habari. 
Tutaendelea kukuletea taarifa juu ya tukio hili 

0 comments:

Post a Comment