Baada ya wasanii wanne kutekwa na watu wasiojulikana, mama mzazi wa msanii ‘Moni’ Fatuma Salehe Awadhi amempiga marufuku mwanae kuendelea na muziki.Bi. Fatuma ameyasema hayo leo akiwa nje ya Kituo cha Polisi cha Osterbay wakati wasanii hao wakihojiwa.“Yani sitaki kabisa mwanangu akitoka aendelee na muziki, bora hata auze nyanya kuliko kuendelea kufanya kazi hii,” amesema.Kwa upande wa Ney wa Mitego alipowasili kituo cha Osterbay amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kukomesha tabia ya utekaji wasanii.“Hii ni faraja kwa kila Mtanzania na shabiki wa muziki. Nadhani hivi ni vitu ambavyo hatujavizoea tangu tunakua kabla kabla ya kuimba muziki, wahusika wanaotakiwa kudhibiti hivi vitu,” amesema Ney na kuongeza.
“Inatakiwa wachukue hatua kabisa sababu tutakako kuwa tunaenda sio kuzuri
maswala ya kutekana hakuna hatujazoeshwa kutekwa tuendelee kujivunia tulichojaaliwa inabidi tuidhibiti hii hali.
0 comments:
Post a Comment