Yasmin
Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake
atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho
kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.
Kwa mujibu wa mtandao
wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati
atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani
atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.
Duru zinasema kuwa mwanamke
Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston
akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.Kwa
sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume
na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu
wawili.
Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana
na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana
kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi
hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.
Aliposikia
kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga
kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.
"Eleby
alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia
ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema
harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya
kijamii.Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa."watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.

"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.

0 comments:
Post a Comment