
STAA wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ameibuka na kusema
hayupo tayari kuzaa na mpenzi wake wa sasa ambaye pia ni msanii, Kulwa
Kikumba ‘Dude’ ingawa anatamani kuzaa mtoto wa kike baada ya mwanaye wa
kwanza wa kiume kuwa mkubwa.
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akichonga na Za Motomoto News, Ester alisema hivi sasa umri unakwenda
na ni vyema akizaa ili kazi ibakie kuwa moja tu ya kulea, huku akiwa
hajui ni mwanaume gani sahihi wa kushiriki naye katika uzazi huo.
“Siwezi kukueleza kwa nini sitaki kuzaa na Dude, labda umuulize
mwenyewe ila kiukweli natamani sana mtoto wa kike kwa sasa, maana huyu
niliyenaye ameshakua mkubwa, anahitaji mdogo wake,” alisema Ester.


0 comments:
Post a Comment