Friday, April 28, 2017

Msanii wa muziki wa miondoko ya Hip hop, Mabeste amefunguka ya moyoni kwa kusema anatamani mtoto wake Kendrick Mabeste aje kupita katika nyayo zake za muziki anazozifanya hivi sasa.

Mabeste amesema atafurahi sana siku moja akaja kumuona kijana wake huyo anajihusisha na muziki kwa kuwa anaamini ataleta changamoto nyingi kutokana na ubunifu atakaokuja nao.
"Natamani nimuone mwanangu Kendrick siku moja anakuja kuwa Rappa mkali, mbunifu na kuleta changamoto katika muziki lakini pia naamini ipo siku atafanya hivyo". Alisema Mabeste
Kwa upande mwingine kijana huyo siku za hivi karibuni ameweza kujinyakulia tuzo ya kwanza shuleni kwao ya kuwa 'Best Baby Boy Photogenic All Star 2017'.

0 comments:

Post a Comment