Saturday, April 1, 2017

BAADA ya hivi karibuni mkewe kujifungua mtoto wa kike aitwaye, An­yagile, msanii wa Bongo Fleva, Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, mtoto huyo amempa mzuka zaidi wa ku­fanya muziki.

Akipiga stori na ShowbizNuh alianza kwa kufafanua maana ya jina la Anyagile kuwa linamaanisha amenikuta baada ya kumpokea, nguvu kubwa anaielekeza kwenye muziki ili apate chochote cha kum­fanya akue.
“Nimefurahi sana kupata mtoto wa kike, mke wangu alishakuwa kwenye uhusiano na wanaume wengi lakini haja­wahi hata kuwabebea mimba lakini kwa muda mfupi amenipa­tia kijike. Kilichobaki sasa hivi ni toa ngoma weka ngoma,” alisema Nuh anayebamba na Wimbo wa Anamer­emeta.

0 comments:

Post a Comment