Msanii Witness Kibonge mwepesi ambaye anatamba na ngoma ya 'Mzuka' aliyoiachia hivi karibuni leo ametoa ya moyoni kwamba muonekano wake wa kiume ulimkosesha kazi katika shirika la UNICEF.
Witness amefunguka hayo leo kwenye 'Heshima ya bongo fleva ya Planet Bongo na kudai kupenda kwake kurap kulimbadilisha maisha hali iliyompeleka kubadili muonekano wake na kuwa na muonekano wa kiume ambao ulimkosesha ajira.
"Mimi nilikua muimbaji kabla sijajua kurap, lakini waimbaji kitambo hicho tulikuwa tunachukuliwa poa hivyo nilihamia Kinondoni ili niweze kukutana na wale ma legend wa kuchana hivyo ule muonekano wa kike wote ukaondoka nikawa kama 'tom boy' kwa sababu ya kutumia muda mwingi na masela" alisema Witness
Witness akaendelea kufafanua kuwa muonekano wake huo wa kiume ulimpelekea kukosa kazi
"Sasa wakati wa kutafuta kazi ukafika nikawa nimepata nafasi UNICEF, CV na Biography yangu ilikuwa safi na viliweza kunibeba sana lakini sasa boss alivyokuja baada ya kuniangalia ilitosha kuniambia hakuna kazi, jinsi nilivyovaa na muonekano wangu na kuanzia hapo ile mentality ya kwamba rap lazima uvae kiume iliondoka ingawa ilinichukua kama miaka miwili kurudia hali ya kawaida" - Witness alisisitiza
Witness aliwahi kuwa katika kundi la Wakilisha lililokuwa limeundwa na marehemu Langa pamoja na Shaa ambao wote walishiriki na kufanya vizuri katika shindano la Coca Cola Pop Star.
0 comments:
Post a Comment