Image
copyrightAFPImage captionSharbat Gula asindikizwa na polisi kuondoka
hospitalini kabla ya kusafirishwa hadi mpakaniMwanamke kutoka
Afghanistan aliyepata umaarufu duniani picha yake ilipochapishwa kwenye
ukurasa wa kwanza wa jarida la National Geographic mwaka 1985 alipokuwa
msichana ametimuliwa kutoka Pakistan.
Hii ni baada yake kupatikana na stakabadhi bandia za utambulisho.Sharbat Gula amefurusgwa kutoka Pakistan baada yake kutumilia kifungo cha siku 15 jela akiwa hospitalini ambapo amekuwa akitibiwa ugonjwa wa hepatitis C.
Hii ni baada yake kupatikana na stakabadhi bandia za utambulisho.Sharbat Gula amefurusgwa kutoka Pakistan baada yake kutumilia kifungo cha siku 15 jela akiwa hospitalini ambapo amekuwa akitibiwa ugonjwa wa hepatitis C.
Yeye na wanawe wanne wamekabidhiwa kwa maafisa wa Afghanistan mpakani.
Anatarajiwa kukutana na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani mjini Kabul.
Sharbat Gula alitoroka Afghanistan ilipokuwa chini ya utawala wa muungano wa Usovieti.
Picha yake kama mkimbizi, ambapo alionekana kuwa na macho makali, iliibuka kuwa kama nembo ya madhara ya vita Afghanistan.
Macho yake yalikuwa na rangi ya kijani, jambo lililomfanya kufahamika kwa jina
Baada
ya kukamatwa kwake eneo la Peshawar, karibu na mpaka wa Pakistan na
Afghanistan tarehe 23 Oktoba, alikiri makosa yote na akapigwa faini ya
rupia 110,000 ($1,100).
Alikabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela miaka kadha.
Pakistan ilianza kuwasaka watu wenye vitambulisho bandia majuzi huku uhusiano wake na Afghanistan na India ukidorora.
Image
copyrightEPAImage captionSharbat Gula, aonekana awali kabla yake
kutimuliwa kutoka PakistanPicha maarufu ya Bi Gula ilipigwa 1984
alipokuwa kambi ya wakimbizi kaskazini magharibi mwa Pakistan.Wakati huo
wanajeshi wa Muungano wa Usovieti walikuwa wameingia Afghanistan.
Mwaka
2002, mpiga picha Steve McCurry alimtafuta na kumpiga picha. Wakati huo
alikuwa anaishi kijiji kimoja Afghanistan akiwa na mumewe na binti zao
watatu.
Baada ya kutokea kwa habari za kukamatwa kwa Bi Gula, Bw McCurry alisema atafanya kila juhudi kumsaidia kifedha na kisheria.
Sharbat Gula alipigwa picha na Steve McCurry (pichani), ambaye miaka 17 baadaye alimtafuta na kumpiga picha nyingine
0 comments:
Post a Comment