Tasnia ya filamu nchini ipo katika mikakati mizito ya kuhakikisha inatokomeza kabisa maharamia wa filamu nchini.
Ikiwa operesheni hiyo inaambatana na kuziifungia filamu za nje ambazo zinatafsiriwa kwa lugha ya kiswahili hapa nchini, filamu ambazo zinasadikika kufanya soko la filamu za hapa nchini kutetereka.
Ikiwa wana Bongo Movie wanaendelea na sakata hilo, mkali kutoka Bongo Flevani, Nikki wa Pili amezua gumzo baada ya kutweet maneno ambayo wengi waliyachukulia kama dongo kwa tasnia ya filamu hapa Tanzania.
Ikiwa ni baada ya kutolea mfano kwamba filamu za Rambo ni maarufu kuliko Rambo mwenyewe, tofauti na hapa nchini ambapo msanii anakuwa maarufu yeye kuliko sanaa yake.

0 comments:
Post a Comment