kumekua
na ripoti nyingi na matukio ambayo inatokea mtu anazikwa kabla hajafa,
hasa sehemu za vijijini sana ambapo hakuna madaktari au wahudumu wa
afya. kwa sheria za tanzania, mgonjwa akifia hospitali basi dakatari
ndio anaruhusiwa kukagua na kuhakikisha kweli mgonjwa huyu amefariki
kabla ya kwenda kuzikwa. elimu hii ya kujua kama mgonjwa bado yuko hai
au amekufa ni vizuri ikatolewa kwa watu wote ili kuepusha matukio hayo
ya kuzika watu walio poteza fahamu tu wakidhani ni wafu.zifuatazo ni
dalili hizo.
kusima
kwa mfumo wa upumuaji;muangalie mtu kifuani kisha kua makini, kwa mtu
aliyepoteza fahamu utaona kifua kinapanda na kushuka lakini kwa mtu mfu
utaona kifua kimetulia kabisa na hakuna dalili za kupumua hata kwa
mbali.
kusimama
kwa mapigo ya moyo; haya unaweza kuyasikia kwa kutumia kifaa maaluma
kwa jina la stethoscope lakini kwa mtu wa kawaida ambaye sio mtaalamu
basi weka sikio lako upande wa kushoto mwa kifua cha mtu na kama
husikiii mapigo ya moyo huyu mtu ni mfu.
msukumo
wa damu; hii kitaalamu inaitwa pulse rate,kwa kutumia vidole vyako
viwili vya mkono wako kandamiza kidogo sehemu ya mkono ambapo kuna
kidole gumba. kwa kawaida utahisi damu inapita na inasukuma vidole vyako
na kama husikii kabisa basi huyo ni mfu.pia unaweza kuweka vidole
shingoni kama wafanyavyo askari mara nyingi kukagua kifo.

angalia jicho; jicho lina duara mbili nyeusi, moja ni kubwa na nyingine
ndogo kabisa kitaalamu tunaita pupil. kwa hali ya kawaida pupil ukipiga
tochi ghafla nasinyaa na ukitoa tochi inapanuka kawaida. sasa kwa mfu
hautaona hayo mabadiliko lakini pia pupil yake itakua imepanuka kuliko
kawaida.angalia tofauti kwenye picha hizi mbili.

kukakamaa
sana; kutokana na kusimama kwa kazi ya mishipa ya fahamu, mfu hukakamaa
sana muda tu baada ya kufa na usipowahi kumnyosha basi anaweza asirudi
kwenye hali ya kawaida.
kuwa wa baridi; inategemea na muda wa kifo lakini mara nyingi masaa nane baada ya kifo mtu huanza kuwa wa baridi sana kuliko kawaida hasa miguuni kutokana na kupotea kwa joto la kawaida la kiumbe hai.
kuanza kutoa harufu kali; vitu laini sana kwenye mwili wa binadamu kama ubongo na utumbo huanza kuoza haraka mtu anapokufa, hivyo harufu kuotekea sehemu zote zenye mashimo kama pua, mdomo, na sehemu za siri huanza kutoka.
kutosikia maumivu kabisa; mfinye sana mgonjwa miguuni au mkononi au sehemu yeyote yenye nyama lakini hautaona ushirikiano wowote.
mwisho; kuna njia zingine za kujua kifo ambazo zinatumia vifaa maalumu na zingine huwezi kuzielewa kama wewe sio daktari, lakini ukiona dalili zote hizo kwa mgonjwa kwa uhakika basi unaweza kusema amefariki japokua ni vizuri kumuita na daktari ahakikishe ila kama ni kijijini sana basi mnaweza kuzika.unaweza kubonyeza maneno ya kijani kwa maelezo zaidi na kupitia blog yangu ya kingereza.
kusimama
kwa mapigo ya moyo; haya unaweza kuyasikia kwa kutumia kifaa maaluma
kwa jina la stethoscope lakini kwa mtu wa kawaida ambaye sio mtaalamu
basi weka sikio lako upande wa kushoto mwa kifua cha mtu na kama
husikiii mapigo ya moyo huyu mtu ni mfu.
msukumo
wa damu; hii kitaalamu inaitwa pulse rate,kwa kutumia vidole vyako
viwili vya mkono wako kandamiza kidogo sehemu ya mkono ambapo kuna
kidole gumba. kwa kawaida utahisi damu inapita na inasukuma vidole vyako
na kama husikii kabisa basi huyo ni mfu.pia unaweza kuweka vidole
shingoni kama wafanyavyo askari mara nyingi kukagua kifo.
angalia jicho; jicho lina duara mbili nyeusi, moja ni kubwa na nyingine
ndogo kabisa kitaalamu tunaita pupil. kwa hali ya kawaida pupil ukipiga
tochi ghafla nasinyaa na ukitoa tochi inapanuka kawaida. sasa kwa mfu
hautaona hayo mabadiliko lakini pia pupil yake itakua imepanuka kuliko
kawaida.angalia tofauti kwenye picha hizi mbili.
kukakamaa
sana; kutokana na kusimama kwa kazi ya mishipa ya fahamu, mfu hukakamaa
sana muda tu baada ya kufa na usipowahi kumnyosha basi anaweza asirudi
kwenye hali ya kawaida.kuwa wa baridi; inategemea na muda wa kifo lakini mara nyingi masaa nane baada ya kifo mtu huanza kuwa wa baridi sana kuliko kawaida hasa miguuni kutokana na kupotea kwa joto la kawaida la kiumbe hai.
kuanza kutoa harufu kali; vitu laini sana kwenye mwili wa binadamu kama ubongo na utumbo huanza kuoza haraka mtu anapokufa, hivyo harufu kuotekea sehemu zote zenye mashimo kama pua, mdomo, na sehemu za siri huanza kutoka.
kutosikia maumivu kabisa; mfinye sana mgonjwa miguuni au mkononi au sehemu yeyote yenye nyama lakini hautaona ushirikiano wowote.
mwisho; kuna njia zingine za kujua kifo ambazo zinatumia vifaa maalumu na zingine huwezi kuzielewa kama wewe sio daktari, lakini ukiona dalili zote hizo kwa mgonjwa kwa uhakika basi unaweza kusema amefariki japokua ni vizuri kumuita na daktari ahakikishe ila kama ni kijijini sana basi mnaweza kuzika.unaweza kubonyeza maneno ya kijani kwa maelezo zaidi na kupitia blog yangu ya kingereza.
0 comments:
Post a Comment