
Hii inayomuhusu mwanamke anayefahamika kwa jina la Nicole ambaye sauti yake imekuwa inasambaa kwenye mitandao akilalamika kuwa staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee anamchukulia mume wake.
Nicole anamtuhumu Vanessa kumchukulia mume wake na kwenda kuishi naye hotelini na kupelekea mume huyo kutokwenda kumuona mtoto wake tangu amezaliwa.
Soudy Brown alimtafuta Vanessa Mdee lakini hakumpata ambapo alimtafuta Nicole ili kujua ukweli na majibu yake yalikuwa haya..“Hiyo sauti siyo yangu, ila nilisikia story tu japo mimi najua ni watu wa karibu sana. So, siwezi kusema anatoka naye maana sijawakamata. Mimi najua wako karibu ni marafiki japo nilimuuliza akaniambia ni dada yake, na, ni kweli baba mtoto hajamuona mtoto tangu azaliwe.” – Nicole.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza..
0 comments:
Post a Comment