Tuesday, April 11, 2017

Kubadilisha matumizi ya majengo mbalimbali imekuwa ni kawaida kwa nchi mbalimbali, watu wameendelea kufikiria namna ya kubadilisha matumizi ya majengo mbalimbali ili kufanya biashara zaidi.

January  2017 nimekutana na haya majengo kutoka sehemu mbalimbali duniani ambayo yalibadilishwa matumizi yake na kuboreshwa zaidi kutoka kuwa magereza na kuwa sehemu kama vile shule na Hoteli.
Gereza la Pentrige, Melbourne Australia 
Hili lilikuwa ni gereza lakini mtu binafsi alinunua eneo hili mwaka 2013 na kubadilisha kuwa makazi ya watu na hotel ya kifahari
   
Centro Civico, Palencia Spain 
Hispania ilibadilisha gereza hili na kuwa kituo cha utamaduni na sanaa
  
Convent of the Penitents, Ufaransa
Gereza hili lilibadilishwa na kuwa shule ya muziki
  
Four Seasons Hotel, Instabul Uturuki
Hii ni hoteli lakini lengo la msingi la kujengwa kwake ilikuwa ni kuwa gereza
  
Hullet House, Hong Kong
Jengo hili lilijengwa mwaka 1881 na lilikuwa likitumika kama makao makuu ya gereza la askari wa majini
  
Gereza la Reading, Uingereza
Wageni wengi wamefika gereza la Reading Uingereza, baada ya kufunguliwa kwa mara ya kwanza ajili ya umma September 2016 kama nafasi ya maonyesho.
  

0 comments:

Post a Comment