Thursday, April 27, 2017

Rais Dkt. John Pombe Magufuli siku ya kesho Ijumaa anatarajia kupokea ripoti ya taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa Umma ambayo itawasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema anasubiri ripoti ya Watumishi wa serikali ambao wanavyeti feki ili awashughulikie huku akidai kuna watu zaidi wa elfu tisa wana vyeti feki.
Rais Magufuli atakabidhiwa ripoti hiyo kesho kwenye ukumbi wa Chimwaga, Dodoma 

0 comments:

Post a Comment