KUFUATIA mambo mengi kumtokea Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ tangu aachie wimbo wake wa Wapo, jamaa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha yake ya kila siku.
Utakumbuka
hivi karibuni NaY alielezea vitisho vya kuuawa anavyovipata kutoka kwa
watu wasiojulikana ambao wanaonesha kutofurahishwa na tamko la Rais Dk. John Magufuli la kutaka aachiwe licha ya wimbo wake kuonekana una ukakasi.
Hata
hivyo, kufuatia tukio hilo, dizaini kama jamaa ameamua kutojichanganya
sana kitaa, badala yake inadaiwa na watu wake wa karibu kuwa, amekuwa
akitulia nyumbani kwake akifanya shughuli za hapa na pale ikiwa ni
pamoja na kufuga kuku wake wa kienyeji.
Kusikia hivyo, mapaparazi wetuwakamfungia safari hadi nyumbani kwake, Kimara Mwisho jijini Darambapo
katika hali ya kushangaza, palikuwa pametawaliwa na ukimya ndipo
baadaye ikabainika kuwa, watu aliokuwa anaishi nao akiwemo mama yake,
wameondoka kwa hofu ya kufanyiziwa.
HUYU HAPA NAY Baada
ya kubisha hodi kwa muda mrefu, alifi ka getini kijana mmoja ambaye
kabla ya kufungua aliuliza maswali kibao ndipo alipokwenda kumuita baba
mwenye nyumba (Nay).
Alipokuja Nay na kuona ni waandishi anaowafahamu akafungua. Akizungumzia maisha yake kwa sasa, msanii huyo alisema:
“Ni
kweli hali yangu ya usalama haipo vizuri, sasa ili kujiepusha na mambo
mengine inanilazimu kukaa nyumbani muda mwingi na kufanya shughuli kama
hizi za kulisha kuku wangu, kuhudumia garden na shughuli nyingie
ndogondogo.
“Kwa
kifupi mimi ni mfugaji mzuri sana wa kuku wa kienyeji, ninao wengi na
wamenizoea kwa kuwa ni wa kienyeji lakini nawalisha kizungu kama
unavyoona.”







0 comments:
Post a Comment