Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego, ameikataa vita ya ulingoni dhidi ya Yusuph Mlela huku vita yao ya kurushiana maneno mtandaoni ikiendelea .
Rapa huyo amedai yeye hana muda wa kupoteza kupigana na msanii wa ‘Bongo Movie’ huku akijitapa kuwa hapangiwi wala hafundishwi jambo analotaka kuongea.
“Mimi ni Baba mwenye watoto, mimi ni mtu mwenye familia. So ukiwa unataka kuniuliza kitu angalia watu wa kuniweka nao ,” Nay alikiambia kipindi cha EA Radio cha EATV.
Aliongeza, “Usiniweka na watu ambao unaona kabisa hiki siyo sawa. Mimi naongea na Bongo Movie wote. Mimi nipo ‘free’ sana nipo huru kuongea jambo lolote. Mimi napenda kuongea ukweli, wewe unaweza kukataa nilichokiongea lakini asilimia kubwa wanaelewa ninachoongea, thats why nikisimama sehemu nikizungumza, watu wanaelewa nazungumza nini, ndiyo maana sijawahi kupindisha, mimi huwa naongea ‘straight’ ndiyo maana kuna watu wananiamini sana,”
Wawili hao waliingia kwenye mgogoro wa kurushiana maneno baada ya rapa huyo kuwaita mataahira wasanii wa filamu walioandamana kupinga filamu za nje ambazo zinadaiwa hazilipi kodi.
0 comments:
Post a Comment