Salum Njwete ‘Scorpion’ akiingia Mahakama ya Mwanzo Ilala, Dar.Kesi ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’, anayedaiwa
kumjeruhi kwa kumchoma visu na kumsababishia upofu Said Mrisho, leo
imeshindwa kuendelea baada ya shahidi upande wa Jamhuri kushindwa
kutokea mahakamani.
Katika viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kama kawaida umati uliokuwa ukitaka kusikiliza kesi hiyo ulifurika mapema asubuhi kutaka kujua kinachoendelea.
Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Ukonga na kuhifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya mahakama hiyo.
Majira
ya saa nne kamili chumba cha mahakama kilikuwa tayari kimeandaliwa kwa
ajili ya kesi hiyo ambapo Wakili wa Scorpion, Juma Nasoro, Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga, Hakimu anayeendesha kesi hiyo,
Frola Haule na makarani wote walikuwa tayari kwenye chumba inapoendeshwa
kesi hiyo wakimsubiri mtuhumiwa huyo apelekwe ili kesi iendelee.
Baadaye
maafande wa magereza zaidi ya nane wengine wakiwa na silaha walimchomoa
Scorpion na kumpeleka kwenye chumba cha mashitaka mbele ya hakimu,
Frola Haule.
Scorpion
akiwa kizimbani, Wakili Katuga aliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo
ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa nane upande wa Jamhuri
kutoa ushahidi wake.
Askari Magereza wakimsindikiza Scorpion kwenda Gereza la Ukonga.
Wakili huyo alisema shahidi huyo alitoa udhuru mahakani hapo kuwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa anaumwa.
Baada ya ombi la wakili huyo, mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo mpaka Mei 2 mwaka huu ambapo Scorpion alirudishwa rumande.





0 comments:
Post a Comment