Saturday, April 1, 2017



Kutoka Kushoto: Meneja wa Songa, Chin, Songa, Sintah (Mdundo Tanzania), Tiddy Hotter na Prisna Nicholaus (Mdundo Tanzania)

Kwa mara ya kwanza, kampuni ya muziki ya Mdundo.com inayowezesha mashabiki kupakua nyimbo mbalimbali za wasanii wa muziki hapa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla, Ijumaa hii, Machi 31, 2017 imefanikiwa kutoa tuzo kwa wasanii ambao wameshinda kutokana na wingi wa upakuaji wa nyimbo zao.

Katika tuzo hizo wasanii waliopata ushindi ni pamoja na Ben Pol ambaye amefanikiwa kuchukua tuzo mbili, Msanii wa bora wa Afropop pamoja na wimbo bora uliopakuliwa zaidi, huku tuzo ya msanii bora wa hiphop ikichukuliwa na Songa. Washindi hao walipata nafasi ya kujumuika pamoja na kupata chakula cha mchana katika maeneo ya Masaki kwenye kiota cha Alcove Restaurant.
Tuzo hizo ambazo zilikuwa zinawaniwa na wasanii mbalimbali, zilikuwa kwenye vipengele vikuu vitatu:
Kipengele cha wimbo ulio pakuliwa zaidi:

Washiriki:

1: Enzi Za Utoto – Songa
2: Forever – Ruby
3: Juu – Jux and Vanessa
4: Kamatia – Navy Kenzo
5: Mahaba Niue – Maua Sama
6: Moyo Mashine – Ben Pol
7: Siwezi – Braka Da Prince
8: Skendo – Mo Music
9: Uzuri Wako – Jux


Kipengele cha Msanii bora wa Hip Hop:

1: Chindo Man
2: Dizasta
3: Gnako
4: Godzilla
5: Nikki Mbishi
6: One The Incredible
7: P The Mc
8: Songa
9: Young Killer


Kipengele cha Msanii Bora wa Afropop:

Washiriki:
1: Barakah Da Prince
2: Belle 9
3: Ben Pol
4: Christian Bella
5: Jux
6: Maua Sama
7: Mo Music
8: Navy Kenzo
9: Ruby
10: Vanessa

Unaweza ukatazama hapa picha za tuzo hizo:


Songa akiwa na Meneja wake, Chin



Tuzo 3 ambazo Ben Pol na Songa wameshinda



Ben Pol akiteta jambo na Prisna Nicholaus wa Mdundo Tanzania



Ben Pol akiwa amezishika tuzo mbili alizoshinda



Prisna Nicholaus kutoka Mdundo Tanzania akimkabidhi Songa tuzo yake



Songa akiwa ameishika tuzo yake ya Mdundo



Producer Tiddy Hotter aliyetayarisha wimbo wa Ben Pol, Phone alimpa kampani Ben katika hafla ndogo ya kukabidhiwa tuzo za Mdundo



Prisna Nicholaus kutoka Mdundo Tanzania akimkabidhi Ben Pol tuzo yake



Prisna Nicholaus (katikati) akizungumza jambo huku Ben Pol na Sintah wakimsikiliza

0 comments:

Post a Comment