Baada ya kuwa kimya kidogo katika tasnia ya filamu hapa Bongo, Wema Sepetu aahidi kutowaangusha watanzania kwa hili jipya linalokuja.
Good Newz ni kwamba, Wema Sepetu pamoja na Gabo, wako mbioni kuwaletea watanzania filamu mpya ya “Heavensent” ambayo itakuwa bora zaidi kwa kuwa Mrembo Wema Sepetu ameahidi kwamba muda huu sio wa mchezo tena, amekuja kuwapa waTanzania kitu ambacho siku zote walikuwa wakikihitaji katika tasnia ya filamu hapa Bongo.
Katika filamu hiyo ya “Heavensent” ambayo imeongozwa na Neema Ndepanya chini ya kampuni ya Fontana Entertainment, Wema Sepetu aliamua kushare baadhi ya picha za Scene ya filamu hiyo huku akiwaahidi watanzania mambo mazuri kutoka kwake.
0 comments:
Post a Comment