Uzinduzi wa akaunti hiyo utafanyika makao makuu ya klabu hiyo yakiongozwa na ofisi ya katibu mkuu wa klabu hiyo , ndugu Charles Boniface Mkwasa .Akizungumzia uzinduzi huo , katibu mkuu wa klabu hiyo amesema wapo katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za ufunguzi wa akaunti hiyo.” tupo katika hatua za mwisho kukamilisha hatuza za ufunguzi wa akaunti hiyo. Akaunti itakuwa na uwazi na kila kinachochangiwa kitaonekana na dhumuni la kufungua akaunti hiyo litasimamiwa vyema . Ni wazo ambalo wadau , mashabiki na wanachama wamelileta na sisi kama uongozi tumelibariki. Hii ni timu ya wanachama hivyo maamuzi yao chanya tunayeheshimu sana . ” alieleza katibu huyo katika mkutano ambao ulikuwa rasmi kuzungumzia safari ya kuondoka kwa Yanga SC kuelekea Algeria kesho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment